Baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya nchini akiwemo Mwana Fa, Izzo Business,Kala Pina pamoja na Judith Wambura 'Lady Jayde' wamehairisha shoo zao ambazo zilikuwa zinatarajia kufanyika mwisho wa mwezi huu kwa sababu ya kifo cha msanii mwenzao Albert Mangwea kilichotokea jana nchini Afrika ya Kusini.
Lady Jayde amesitisha shoo yake ya uzinduzi wa albamu yake ya 'Nothing but Trust' iliyokuwa inatarajia kuzinduliwa mwisho mwa wiki hii jijini Dar es Salaam kwa kufwatia kifo cha msanii mwenzake Albert Mangwea aliyefariji jana nchini Afrika ya Kusini
Mwana Fa naye alitarajia kufanya onyesho lake alilolipa jina la The Finest mwishoni mwa wiki hii amejikuta akiahirisha shoo hiyo kwa sababu ya msiba wa msanii mwenzao
Kwa upande wake Izzo Business alieleza sababu ya kuahirisha shoo hiyo, alisema kuwa hawezi kuendelea na ratiba ya shoo hiyo wakati yupo katika wakati wa majonzi kwa kumpoteza msanii wao ambaye pia ni rafiki yao mpendwa .
0 comments